Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Bwana harusi akataliwa kuoa siku ya harusi

on

Heka Heka ya Leo November 9 2016 kwenye leo Tena ya Clouds FM ni kuhusu Bwana harusi aliyekataliwa kuoa dakika za mwisho za harusi huku taratibu zote zikiwa zimefatwa kwa kutolewa barua na mahari huku bibi harusi akiwa ameshafanyiwa kitchen party na mama yake.

Imeelezwa kuwa sababu iliyopelekea bwana harusi kukataliwa ni kutokana na baba mzazi wa bi harusi kutokushirikishwa kwenye chochote na mama wa bi harusi mpaka siku hiyo ya ndoa alipopewa taarifa na akaamua ndoa isifungwe.

>>>”Nilipanga mwanangu aolewe lakini baba mtu nikawa sijamshirikisha niliwaambia  ndugu zangu baba mtu kakataa kasema haolewi ndio basi, tumetengana siku nyingi mimi na baba yake na barua ilivyopelekwa hatukumpelekea, mtoto nimemlea mwenyewe lakini huwa anaenda tu kwa baba yake kumsalimia”Mama wa Bibi Harusi

>>>”Baba kapigiwa simu akasema mtoto asiolewe basi tukakubali ndoa ivunjwe, mimi sijui wanajuana wenyewe wazazi, ndio tushamalizana tena zawadi zangu nimepewa kama mwali wa kawaida  sio bi harusi tena”- Bibi Harusi

Full stori iko hapa. Bonyeza play kusikiliza

 

VIDEO: Walichokifanya Msami na Hamadai kwenye jukwaa la FIESTA2016 Leaders Club Dar es salaam, Tazama hapa

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement