Tangaza Hapa Ad

Mix

Habari 5 ‘HOT’ kwenye TV za Tanzania August 27 2016

on

Habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya August 27 2016 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano kubwa kupitia TV za Tanzania.

Habari kutoka Clouds TV

Jeshi la Polisi laongeza nguvu 

Msako wa majambazi msitu wa vikindu unaendelea ambapo maaskari zaidi ya 80 kuungana na wenzao walioko katika msitu huo ili kuongea nguvu ingawa idadi ya vifo na waliokamatwa bado haiwekwa wazi.

 >>>kwa raia wakawaida ukimwambia ni mapambano ya silaha anayaona makubwa lakini mapambano ya silaha kwetu Polisi ni ya kawaida sana na ndomana askari polisi akifa kwa kwa kupigwa risasi sisi tunaona ni jambo la kawaida‘- kamishna wa Polisi kanda maalum, Simon Sirro

NEWS

Habari kutoka Clouds TV

Jeshi la JWTZ wamefanya usafi baadhi ya maeneo ya jiji la Dar e salaam kama sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 52 ya jeshi hilo tangu kuanzishwa kwake.

NYUZI

Habari kutoka ITV

Jubilee miaka 50 ya ndoa ya Rais mstaafu Benjamin William Mkapa, Rais John Pombe Magufuli ameongea haya

>>>’ Katika siku hii ambayo tumeadhimisha miaka hamsini ya ndoa yenu, na mimi nimepata muujiza wa tofauti leo kwasababu leo nimeshikana mkono na Mhe. Lowassa, tumezunguka kampeni zote sikuwahi kukutana nae kwahiyo harusi ya leo ni muhimu sana kwahiyo miujiza katika ndoa yenu ni muujiza kwetu sisi wanasiasa pia ambao nikiri kweli tulikuwa na ushindani mkubwa‘ – Rais Magufuli

NYUU

Habari kutoka TBC 1

Tanzania ipo tayari kujifunza mpango wa kujitathmini kiutawala bora barani Afrika.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema viongozi wa Afrika hawana budi kukubaliana na kuungana kutafuta suruhisho katika ushindani wa kibiashara kukuza uchumi wa nchi husika.

nyululu

Habari kutoka ITV

Uharibifu sokoni 

Manispaa ya ilemela yaamrishwa kulipa fidia wajasiriamali wa matunda yalioharibika baada ya uharibifu sokoni hapo.

nyoli

ULIKOSA KUITAZAMA VIDEO YA KAMANDA SIRRO ALIPOSEMA ‘KUNA WATU TUMEWAKAMAA KATIKA TUKIO LA MAUAJI YA POLISI’? UNAWEZA KUITAZAMA VIDEO NIMEKUWEKEA HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement