Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Huddah asema Vera Sidika sio chanzo cha yeye kutokuja Wasafi Beach Party

on

Vodacom Wasafi Beach Party ilifanyika weekend iliyopita Dar es salaam ambapo WCB inayoongozwa na Diamond Platnumz ilifanikisha party hiyo na kuwaleta kwenye stage wageni mbalimbali akiwemo mwimbaji Kcee wa Nigeria na Warembo Fabiola (Uganda) na Vera Sidika (Kenya)

Wengi walikua wanasubiria itakuaje baada ya Mrembo wa Kenya aitwae Huddah kutotokea kama alivyotajwa kwenye list ya watakaokuwepo na wengi walikua wanasubiria kuona itakuaje Huddah akiwa kwenye jukwaa moja na Vera ambao wamekua wakitajwa kwamba hawapatani.

screen-shot-2016-12-28-at-10-43-32-am

Fabiola, Vera akiwa na friends na wakali kutoka The Industry.

Baada ya Huddah kutokutokea maneno yalizuka kwamba hajatokea sababu hakutaka kukutana kwenye tukio moja na mtu ambaye hapatani nae yaani Vera, sasa millardayo.com imempata Huddah ambae amesema Vera Sidika sio chanzo cha yeye kutokuja Tanzania.

Sijali kuhusu mtu yoyote, sijali kuhusu sijui nani alikuwepo nani hakuwepo hiyo sio biashara yangu ila kama mtu hakulipii bili zako kila mwezi hawezi kukutishia maisha, pili… kilichotokea ni mimi tu na WCB hatukuelewana malipo na nikaona wameongeza watu wengine‘ – Huddah

Ukweli ni kwamba sikuacha kuja Tanzania sababu ya kuogopa au kutotaka kuwepo kwenye event moja na Vera, mimi mwenyewe nilipost hilo tangazo kwenye page yangu na hiyo inamaanisha simuogopi binadamu yeyote na wala sijali‘ – Huddah

screen-shot-2016-12-28-at-10-43-45-am

Walivyonaswa Vera Sidika na wenzake kwenye Vodacom Wasafi Beach Party 2016

Kwa wanaosema sikuja sababu ya Vera Sidika kuwepo hapo, kwani ni siku gani Vera amenipigia simu na kuniuliza kama nimekula au nililala vipi? hamna…… so yeye sio sababu ya mimi kutokuja, ukweli ni kwamba nilitaka malipo ya pesa nyingi zaidi ili kuja Tanzania‘ – Huddah

Huddah alialikwa pia kwenye Zari All White Party iliyofanyika Dar es salaam May 2015 na akaja mpaka Dar lakini hakufika kwenye tukio lenyewe ambapo alipofanya Interview kwenye OnAIR with Millard Ayo alijibu ni kwanini.

Alisema ‘Nilikua na furaha na nikawa tayari kuhudhuria party lakini baadae nikakaa nikabadilisha tu mawazo na nilikua sijisikii vizuri ndio sababu sikuja kwenye party, nilikua hotelini chumbani kwa Diamond na Zari na niliwaambia

ULIIKOSA VODACOM WASAFI BEACH PARTY? TAZAMA KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement