Top Stories

Watu 11 washikiliwa na polisi kwa kuwanyanyasa ‘wachawi’

on

Nchini Tanzania ni kawaida kusikia kesi za watu mbalimbali kupigwa na wengine kuchomwa moto na wananchi pindi wanapohisiwa kujihusisha na masuala ya ushirikina.

Kutoka nchini India, Jeshi la Polisi nchini India limewashikilia watu 11 wakazi wa Jimbo la Jharkhand Kaskazini baada ya kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji wanawake wawili kwa madai ya kuwa wanajihusisha na ushirikina.

Inaelezwa kuwa wanawake hao ambao ni mama na binti yake walivuliwa nguo na kupitishwa mitaani wakiwa uchi na mwishowe kulazimishwa kula kinyesi cha binadamu.

Kwenye mahojiano na Shirika la Utangazaji la BBC binti huyo ameeleza kuwa wamesigiziwa kusambaza ugonjwa katika kijiji chao kutokana na uchawi, jambo alilosema sio kweli.

Mwanamitindo maarufu Nchini aliyealikwa Ikulu ya Uingereza

Maamuzi ya Mahakama Dodoma kuhusu Kesi ya NABII TITO

 

Soma na hizi

Tupia Comments