Tangaza Hapa Ad

AyoTV

HEKAHEKA: Utata kifo cha mtoto aliyefariki kwenye mazingira ya shule

on

Leo December 6 2016 kupitia hekaheka ya Leo Tena Clouds FM, Geah Habib ametuletea hili tukio la kifo cha mtoto ambaye amefariki akiwa shuleni Morogoro.

Tukio hilo limetokea kama wiki tatu zilizopita, mtoto aliyefariki alikuwa na miaka minane na alikuwa akisoma darasa la tatu, walimu wanadai mtoto alitumbukia kisimani, wazazi hawakubaliani na sababu ambayo wameambiwa kuwa imepelekea kifo cha mtoto wao.

>>>’walimu wanasema ametumbukia kwenye kisima akawa amefariki eti alikuwa anatembea na mwenzake, wanasema wenzake walikuwa wamelala yeye ametoroka na mwenzake wamekimbia kwenda kucheza lakini ukiangalia sio kweli ukiangalia mtoto mwenyewe sio mtundu’:-Mzazi wa mtoto

>>>’Wazazi wangu wakawa wanatoka kwenda kuuona ule mwili, maafisa upelelezi na walimu wakawazuia kwenda kuangalia ule mwili, ndio wakina mama wakawa wameforce kwenda kuuangalia mwili wa mtoto wamekuta vile alivyo mwembamba hana maji, siunajua mtu akifa na maji anajaa tumbo hamna kitu’:-Mzazi wa Mtoto

Bonyeza play hapa chini kusikiliza full story

VIDEO: Wezi walivyokamatwa wakifukua makaburi, Bonyeza play hapa chini kuitazama

VIDEO: Wagonjwa wa kipindupindu waongezeka, sita wamefariki ndani ya mwezi November mwaka huu

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement