Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Mwanamke atoweka aacha mtoto mchanga, alidai anafuata deni lake

on

September 15 ndani ya Leo Tena ya Clouds FM 88.5 Dar es salaam, Mtangazaji Geah Habib amekutana na mkasa wa dada mmoja kutoka Kigogo Luhanga, Dar es salaam baada ya kutoweka nyumbani baada ya kupigiwa simu na mtu aliyekua anamdai pesa kwamba aende akachukue pesa zake.

Dada huyo aliaga nyumbani na kumuacha mtoto wake wa miezi mitano na hakurudi nyumbani huku simu ya marehemu ikitumika kutuma meseji na mtu asiyejulikana kuwa dada huyo amefariki bila kueleza yuko maeneo gani. 

>>>Alipigiwa simu mida kama saa 7 akawa anasema kwamba anataka kuwahi kuna mtu alikuwa anamdai hela yake akasema nikichelewa sitamkuta, mama akamuuliza unaenda wapi? akadai naelekea Tip Top ile kutoka mama akamwambia rudi kwanza mnyonyeshe mtoto akamnyonyesha;-Mdogo wake

>>>Alipoondoka aliondoka jumla hakurudi tena ila mida ya saa 12 mimi nikapokea meseji kwamba mwenye simu hii bahati mbaya, Ikaingia kwa mtu mwingine tena mwenye simu hii hatuko naye ila kama mnamtaka mumfate Tumbi.” ;-Mdogo wake

Licha  ya ndugu zake kwenda Tumbi hawakumpata na wakajaribu hospitali zote bila mafanikio

Nimekurekodia mkasa mzima kwenye sauti hii hapa. Bonyeza Play kusikiliza.

ULIIKOSA HII YA SHETTA KUWAHI KUOSHA GARI LA STAR WA BONGO FLEVA? ITAZAME HII HAPA.

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement