Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Mume amuua mke wake kisa mali za urithi za mume wa kwanza..

on

October 2o, 2016 Kupitia Leo Tena ya Clouds FM imekutana na story ya mwanaume mmoja kutoka Kiwalani jijini Dar es salaam inasemekana amemuua mke wake kisa kikitajwa kuwa ni ugomvi wa mali za urithi za mume wa kwanza wa mwanamke aliyeuawa.

Inaelezwa kwamba wanandoa hao walikua na ugomvi wa mara kwa mara na imetokea mara nyingi masheikh wakajaribu kuwasuluhisha pamoja na mama wa marehemu lakini bado hakukua na suluhu. Siku ambayo aliuawa huyo mwanamke alikuwa anatokea nyumbani kwa mama yake mzazi.

>>>Jumapili walikuja na mume wake lakini wakawa na mabishano marehemu akawa anamwambia mwenzie nipe talaka yangu kwasababu unanipiga sana mimi nimechoka, leo mjomba wangu yupo na mama yupo naomba talaka yangu halafu ukanipe vitu vyangu pamoja na pikipiki za mume wangu ambaye alikua polisi ili niweze kuwalea wanangu. Mwanaume akasema mimi sitoi talaka mpaka nihakikishe umekufa au nimekufa mimi unizike au nikuzike wewe:- Mama wa Marehemu

Kupata stori kamili bonyeza Play hapa chini.

ULIMISS UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO OCTOBER 20? NIMESHAYAWEKA HAPA 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement