Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Jamaa katapeli, katumia njia ya msiba, kahakikisha mpaka kaburi limechimbwa

on

September  7 2016 kupitia Hekaheka ya Clouds FM Geah Habib amekutana na hii iliyotokea Mburahati Dar es salaam ambapo Jamaa aliyewahi kutapeli msikitini mwezi wa Ramadhani akidai kutaka kufuturisha.

Sasa jana September 7 2016 kaenda tena maeneo ya Mburahati ambapo ameefanya utapeli wa aina yake kwa kuwachimbisha watu kaburi na kuwaibia simu na kutokomea, kama hukupata nafasi ya kuisikiliza usijali millardayo.com imekurekodia full stori kutoka kwenye Hekaheka ya leo.

Moja ya mama waliotapeliwa matofali ya kujengea kaburi anasema……>>>aliomba simu yangu wakati vijana wanapeleka matofali akaenda, akongea kuulizia kuhusu mpishi, akawa anauliza fundi mzuri tunampata wapi, akasema ngoja nimwangalie kuna kijana yuko hapa nyuma akaondoka na simu sikuwa na wasiwasi kwa sababu kuna kijana alikuja naye

>>>vijana wangu walirudi kuchukua trip nyingine ya tofauli wakaniambia umeshachukua hela nikasema bado wakasema chukua kwanza hela, namsubiri hakutokea, nikachukua simu nyingine nikapiga simu yangu haipatikani, nikamuuliza yule mwenzie akasema mimi nilikutana naye njiani akaniuliza tofali nzuri nikaja naye

Unaambiwa katapeli mwenye bodaboda, mwenye gari lililokuwa linachukua tofali, mama muuza chai, muuza nyama na mchele.

Kusikiliza full stori, bonyeza play hapa chini

 
ULIKOSA HIZI NYUMBA WALIZOJENGEWA YAMOTO BAND NA MENEJA WAO SAID FELA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement