Biko


Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Mama awaua watoto wake kwa kisu Mbeya, yeye asema hakumbuki kitu

on

October 11, 2016 ndani ya Leo Tena ya Clouds FM, Mtangazaji Geah Habib akiwa Jijini Mbeya amekutana na Heka Heka kuhusu Mama ambaye aliamua kuwachoma kisu watoto wake wawili na kuwauwa kisha akataka kujiua na yeye lakini lengo lake halikufanikiwa.

Mama huyo aliokolewa na wasamaria wema na kukimbizwa Hospitali ambako anatibiwa mpaka sasa, japokuwa kwa mujibu wake hakumbuki kilichotokea na alipoulizwa sehemu walipo watoto wake alidai wameenda shule.

>>>Sikumbuki kitu dada angu nnachokumbuka tulikuwa kwenye kesi ya kifamilia ila sijui tumefikaje hapa mimi sijui nani aliwachoma visu watoto wangu, sikumbuki hata mimi nani kanichoma kisu watoto wako shuleni na baba yao sijui yuko wapi:- Mama aliyeua watoto

>>>Alikuja akiwa hajitambui kabisa na hata waliomleta walikua hawajui nini chanzo ila baadaye tukapata taarifa kwamba walikuwa na matatizo ya kifamilia na kwamba upande wa mwanaume wanadai kwamba wale watoto sio wa kwake akakasirika na kwenda kulala Guest House na huko ndio aliwachoma kisu watoto wake na yeye akajichoma pia akatoke nje ili agongwe na gari lakini watu wakamuwahi na kumleta hapa: Nesi aliyempokea

Unaweza kusikiliza full stori  kwa kubonyeza play hapa chini

ULIMISS SABABU ZA WIZARA YA AFYA KUNUNUA MADAWA INDIA NA SI KENYA? WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AMEELEZA HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement