Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Aishi na wanawake wawili chumba kimoja, alimdanganya mkewe ni dada yake

on

December 8 2016 kupitia kipindi cha Leo Tena  cha Clouds Fm Geah Habibu ametuletea Hekaheka inayotokea Dar es Salaam, Jamaa mmoja ambaye yeye anaishi na mkewe alimdanganya mkewe kwamba ana dada yake ambaye ana matatizo kwa hiyo akamuomba mkewe wakae naye pale nyumbani, mke wake alimkubalia lakini mke anasema akaona mambo hayaendi kama kweli ni mtu na dada yake.

Geah Habib aliongea na majirani ambao wamekuwa wakiamua ugomvi……>>>Walishagombana usiku tukaenda kuamua, yule mwanaume akaanza kujitetea kuwa yule alikuwa ni mwanamke wake wa mara ya kwanza kuna matatizo yalimtokea akamuomba mkewe waaishi naye akawa amekubali’-Jirani 

‘Tunalala kitandani mimi na mume wangu yule wifi yangu analala chini, nikishituka usingizini nakuta mume wangu amelala na dada yake chini, siku nyingine mume wangu ananituma dukani nikirudi nakuta wamefunga mlango nagonga mpaka wakija kufungua unaona tu jinsi ambavyo wametoka kufanya mapenzi’-Mke wa jamaa

Bonyeza play hapa chini kusikiliza full story

AUDIO: Taarifa ya Jeshi la polisi kuhusu kukamatwa kwa mama aliyekuwa akimtesa mtoto wa mwaka mmoja, Bonyeza play hapa chini kusikiliza 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement