Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Jamaa afumwa akimbaka mbuzi, atoa sababu

on

Hekaheka ya leo September 21, 2016 imetokea Moshi Mkoa wa Kilimanjaro ambapo kupitia Leo Tena ya Clouds FM Geah Habib  amekutana na hii ya mbuzi aliyebakwa kwa masharti ya mganga. Tukio hilo limefanywa na kijana ambaye anadai alikwenda kwa mganga wa kienyeji ili kupata dawa za kuwa tajiri ndipo akapewa masharti ya kufanya tendo la ndoa na dada yake wa kuzaliwa au afanye tendo hilo na mnyama.

Akielezea tukio hilo Mlinzi wa eneo alipobakwa Mbuzi huyo anasema……..>>>’Jana jumapili alikuja saa nane za usiku akanikuta nimekaa kwenye viti hivi akaniuliza umelala? nikamwambia eh nimelala asijue kama namtega akazunguka na kuingia kwenye zizi la mbuzi na mbuzi wakawa wanakimbia, nikazunguka kwenda kwenye zizi nikasikia mbuzi analia’

Nikamuona ameinama karibu na mbuzi nikamulika tochi na kumuuliza Sangao unafanya nini akashtuka na kulalia tumbo kisha akaanza kuomba msamaha, nikamwambia ukikimbia nakupiga mkuki na ukirua fensi nakupiga mishale‘:Mlinzi.

Baada ya kukamatwa na kubanwa jamaa huyo alijitetea kwamba alitumwa na mganga aende akafanye mapenzi na dada yake wa kuzaliwa alishindwa kufanya hivyo ndipo mganga akamwambia atafute mnyama akafanya naye tendo hilo.

FULL STORI IKO HAPA MTU WANGU, BONYEZA PLAY KUSIKILIZA.

ULIPITWA NA HII TAARIFA YA AJALI YA BASI LA SUPER SHEM MWANZA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement