Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Mashuhuda wasimulia mtu asiyejulikana kuingilia akina mama usiku Shinyanga

on

September 19, 2016 kupitia HEKAHEKA ya Clouds FM, wametuletea hii inayotokea Shinyanga kuwa mtu asiyejulikana kuingia kwenye nyumba za watu usiku na hasa kwa wanawake.

Hii imetokea kijiji cha Meregani, Shinyanga ambako inaelezwa kuwa kumekuwa na matukio ya mtu asiyejulikana kuingia kwenye majumba ya watu nyakati za usiku kisha kufanya matukio ikiwemo wizi, uharibifu wa vitu pamoja na wale wanaodai kuwa wamekuwa wakiingiliwa kimwili na mtu huyo.

>>>Ile siku ya Jumamosi kuamkia Jumapili mida ya saa 10 usiku, niliamka nikatoka nje nikaona kuna mtu barabarani anapita halafu akasimama karibu na zizi la ng’ombe langu, nikamwangalia na yeye akaniangalia nikakaa muda kidogo nikasema niingie ndani yeye akaanza kuja nyumbani kwangu nikajua ni vijana wangu;-Shuhuda

>>>Nikamuona anaendelea tu kuja nikachungulia dirishani nikamuangalia vizuri nikaona sio kijana wangu, nikafunga mlango akaanza kuchungulia dirishani akaniona niko sebuleni na tukaonana kwa macho, nikaamua kuingia chumbani nikamuamsha mzee. Asubuhi ilipofika tukasikia tukio kuwa kuna mama mmoja anasema ameingiliwa na mtu:- Shuhuda

Full stori unaweza kusikiliza kwa kubonyeza play hapa chini

ULIKOSA HII YA ADAMU MCHOMVU BAADA YA KUINGIA BUNGENI MARA YA KWANZA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement