Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: ‘Scorpion’ mwingine aibuka Sinza DSM, anajiita Van Damme

on

Leo January 19 2017 kupitia Leo tena ya clouds FM Mtangazaji Geah Habib ametuletea hekaheka kutokea mitaa ya Sinza makaburini Dar es salaam.

Hekaheka hiyo ni kuhusu jamaa ambaye amekuwa akifanya matukio ya uhalifu ikiwemo kuchukua mali za watu kibabe kama vile simu, jamaa huyo anajiita ‘Van Damme’. Wananchi wa eneo hilo wamesimulia kuwa ‘Van Damme’ akifika maeneo hayo maduka yanafungwa na madereva bodaboda wanamkimbia……..

‘Amani hakuna huu mtaa yaani ikifika saa moja, yeye ni saa moja hadi saa nne mwisho anaondoka hata wale madereva bodaboda na tax wakimuona amefika wanamkimbia mpaka atakapoondoka ndio wanarudi’;-Mwananchi

Yupo Van Damme jina lake halisi Ayub nilisharipoti polisi nikawaelezea wakasema walimtoa kwa makubaliano kwamba akitoka asifanye matukio, tangu atoke hawajapata ripoti yoyote ya matukio na wao hawawezi kumkamata bila ya kuwa na ripoti yoyote’;Mjumbe 

‘Serikali wanamjua vizuri kwa sababu kashafanya matukio huko nyuma tena makubwa makubwa na amekaa ndani muda mrefu nafikiri mwaka au miaka miwili katolewa ndio huyo yuko mtaani anajulikana, ni familia ambayo tunaijua na mzazi wake tulikuwa tunamfahamu, Serikali inamjua ila inataka watu waende wakaripoti‘;-Mjumbe

Bonyeza play hapa chini kusikiliza Full Stori

HEKAHEKA: Baada ya mazishi wanafamilia wakuta mwili wa marehemu chumbani 

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement