Michezo

Luka Modric hatimae kavunja rekodi ya Ballon d’Or na kuungana na Kaka

on

Staa wa Real Madrid na timu ya taifa ya Croatia Luka Modric amefanikiwa kuingia kwenye headlines na kuweka historia mpya kufuatia ushindi wake wa tuzo ya Ballon d’Or 2018 na kumaliza utawala wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ambao wamekuwa wakitawala na kupokezana tuzo hiyo kwa miaka 10.

Modric mwenye miaka 33 anaendeleza kuwa na msimu mzuri akiisaidia Croatia kufika fainali ya Kombe la Dunia 2018 na kuisaidia Real Madrid kushinda taji la UEFA Champions League msimu wa 2017/2018, Modric sasa anakuwa mchezaji wa pili katika historia kuwahi kushinda tuzo ya Ballon d’Or mbele ya Ronaldo na Messi baada ya Ricardo Kaka wa Brazil kufanikiwa kufanya hivyo mwaka 2007.

Washindi wa tuzo za Ballon d’Or 2018 ni Luka Modric kwa wanaume na wanawake ni mshambuliaii wa Lyon na Norway Ada Hegerberg wakati Mbappe akishinda tuzo ya mchezaji bora mwenye umri chini ya miaka 21 ‘Kopa Trophy’

Luka Modric ameshinda tuzo ya Ballon d’Or akiwa na point 753 akifuatiwa na Cristiano Ronaldo aliyepata point 476, Antoine Griezmann nafasi ya tatu kwa kuwa na point 414 wakati Kylian Mbappe nafasi ya nne kwa kuwa na point 347 na namba 5 ni Lionel Messi aliyepata point 280.

Luka Modric na familia yake

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments