MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Mvua zitaendelea kunyesha hadi kesho

on

Leo April 16, 2018 Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimezidi kusababisha adha kubwa kwa watu wengi huku kukiwa na uharibifu wa miundombinu katika maeneo kadhaa.

Tayari watu watatu wamethibishwa kupoteza maisha kutokana na mvua hizo.

Taarifa ya Mamalaka ya Hali ya hewa imesema mvua hizi zitaendelea hadi kesho Jumanne.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dr. Agnes Kijazi amesema, โ€œMvua itaendelea kunyesha na hii inatokana na kipindi hiki kuwa na mvua kubwa juu ya wastani.โ€

Dr. Kijazi amesema kwa kawaida March na April na zaidi April mvua huwa kubwa juu ya wastani.
Ametoa wito kwa wananchi akisema, โ€œTayari tumeshuhudia maeneo ya bondeni hali ilivyo, kwa hiyo wachukue tahadhari na si wananchi wa bondeni pekee hata maeneo mengine.โ€

BALAA LA MVUA DAR!! Ndege ikipita kwenye maji kupaa

Soma na hizi

Tupia Comments