AyoTV

TFF imetangaza adhabu kwa makamu wake wa Rais TFF

on

Shirikisho la soka Tanzania TFF leo limetangaza adhabu ya makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura anayetuhumiwa kwa makosa matatu, moja kupokea pesa za TFF isivyo halali, kugushi na kushusha hadhi ya TFF.

Baada ya kamati ya maadili ya TFF kukaa jana Jumatano ya March 14 2018, leo kamati ya maadili imefikikia maamuzi ya kumfungia maisha Michael Richard Wambura kujihusisha na soka baada ya kukutwa na hatia katika makosa yote matatu.

 

Wambura amekutwa na hatia katika tuhuma hizo kwania ametumia nafasi yake ya umakamu wa Rais ambaye kikanuni ni mwenyekiti wa kamati ya fedha ya TFF kuidhinisha malipo kinyume na utaratibu.

UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu baada ya sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry

Soma na hizi

Tupia Comments