Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Hawa ndio wakali wa Ndondo Tanzania nzima

on

Baada ya leo February 21 2018 kushuhudia fainali ya Ndondo Super Cup ikiwakutanisha Bingwa wa Ndondo Cup 2017 mkoa wa Dar es Salaam Misosi FC na Goms United ambao wageni wa heshima katika michuano ya Super Cup.

Club ya Misosi FC imefanikiwa kuibuka wakali wa soka la mtaani maarufu kama Ndondo Cup Tanzania nzima, Misosi FC leo imefanikiwa kuifunga kwa mara nyingine tena Goms United kwa goli 1-0 katika mchezo wa fainali ya Ndondo Super Cup ikiwa ni miezi michache imepita toka watwae taji la Ndondo Cup mkoa wa DSM.

Ushindi huo umeifanya Misosi FC kuwa ndio Mabingwa wa kwanza wa kihistoria wa michuano ya Ndondo Super Cup, nikukumbushe tu Super Cup ndio kwa mara ya kwanza imefanyika mwaka huu kwa kuzishirikisha timu Bingwa za mikoa za michuano ya Ndondo Cup ambazo ni Itezi United kutoka Mbeya, Mnadani FC ya Mwanza na Misosi FC na Goms United za DSM.

Soma na hizi

Tupia Comments