Michezo

Yanga SC imepoteza point mbili uwanja wa Taifa Nov 4 2018

on

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania bara Dar es Salaam Young Africans walikuwa wenyeji wa club ya Ndanda FC ya Mtwara uwanja wa Taifa Dar es Salaam November 4 kucheza game yao ya Ligi Kuu, Yanga ambao walikuwa na viporo michezo miwili kabla ya kucheza na Ndanda FC November 4 game yao ya 10 ya Ligi Kuu.

Yanga wakiwa uwanja wa Taifa wameenda kinyume na matarajio ya wengi kuwa watavuna point tatu kirahisi kutoka kwa Ndanda FC ukizingatia ni timu ambayo ina hali mbaya kiuchumi kwa sasa na haipo hata TOP 10 katika msimamo wa Ligi, hivyo wengi hawakutazamia kuwa italazimisha sare ya 1-1 na Yanga.

Ndanda FC ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 16 kupitia kwa Nassor Hashim kabla ya dakika 18 baadae yaani dakika ya 24 Yanga wakasawazisha goli hilo kupitia kwa Jafary Mohamed, matokeo hayo yameifanya Yanga kuvuna point moja na kuziacha mbili, hivyo wapo sawa na mtani wao Simba wakiwa na point 26, Yanga akiwa na kiporo mchezo mmoja hadi sasa akicheza game 10, Ndanda wapo nafasi ya 14 wakiwa na point 13 walizovuna katika game 13.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments