Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kitu Msuva kaandika baada ya kusikia Mahadhi kapiga magoti kuomba msamaha

on

Siku moja baada ya Juma Mahadhi kuomba msamaha kwa viongozi wa Yanga na mashabiki ambao wamekuwa wakilalamika kuwa ameshuka kiwango kwa uzembe.

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga ambaye anacheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe huu baada ya kuona Juma Mahadhi kaomba msamaha kwa kupiga magoti.

#Neno Msamaha , Nisamehe sio Ujinga muhimu umejua wapi umeteleza Naimani Unakipaji kikubwa sana Endelea kuamini kwamba unaweza No time to waste Brother Hongera kwa kutambua ilo naimani wewe ni Champion Endeleza mapambano Mdogo wangu usonge mbele uje ufike Nilipo na Zaidi Nafasi bado Unayo @jumamahadhi21 Twende tuisogeze Tanzania Yetu ?

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Juma Mahadhi Jumanne January 3 2018 aliandika ujumbe wa kuomba radhi mashabiki na baadae wakati wa game ya Mapinduzi Cup ya Yanga dhidi ya Mlandege alifunga goli na kupiga magoti ikiwa ni ishara ya kuomba msamaha mbele ya mashabiki uwanjani hapo.

Juma Mahadhi alipopiga magoti kuomba msamaha Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments