PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Ni Okwi na Pluijm ndio wababe wa TPL mwezi October

on

Mshambuliaji wa Simba ya Dar es Salaam, Emmanuel Okwi amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi October wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019, Okwi anayecheza nafasi ya ushambuliaji, alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Yahya Zayd wa Azam na Eliud Ambokile wa Mbeya City.
Mwezi October ni timu 18 zilicheza michezo mitano kila moja,  isipokuwa Simba na Yanga zilizocheza mechi nne, katika michezo hiyo minne ambayo Simba ilicheza, Okwi raia wa Uganda alitoa mchango mkubwa kwa kupata pointi 12  kwa kushinda michezo yote na kumaliza ikiwa nafasi ya pili.
Okwi kwa mwezi October amefunga mabao 7, matatu akifunga katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 5-0, kwa upande wa Ambokile naye alitoa mchango mkubwa kwa Mbeya City kufanikisha kupata pointi 11 baada ya kushinda michezo mitatu na kutoka sare miwili na kushika nafasi ya nane katika msimamo, akifunga mabao manne.
 Kuhusu Zayd alitoa mchango mkubwa kwa Azam akifunga mabao matatu katika michezo mitano ambayo Azam ilicheza ikishinda yote na kupata pointi 15 ikishika nafasi ya kwanza, pia Kamati ya Tuzo, imemchagua Kocha wa Azam FC, Han Pluijm kuwa Kocha Bora wa mwezi Oktoba akiwashinda Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems na Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nsazwarimo.
Pluijm aliiongoza timu yake kupata pointi 15 baada ya kushinda michezo yote mitano iliyocheza na kushika nafasi ya kwanza, huku Aussems akiiongoza Simba kushinda michezo yote minne iliyocheza hivyo kupata pointi 12 na kushika nafasi ya pili, wakati Nsazwarimo alipata pointi 11 akishinda michezo mitatu na kutoka sare mitatu akiiwezesha timu yake kupanda hadi nafasi ya nane.
IMETOLEWA NA TFF
Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19
https://youtu.be/6R4CaF320mA

Soma na hizi

Tupia Comments