Michezo

Ukimuuliza Oscer kucheza kwake China kutafanya aikose World Cup 2018?

on

Moja kati ya stori zinazochukua headlines kwa March 13 2018 ni pamoja na stori ya kiungo wa zamani wa Chelsea raia wa Brazil Oscer ambaye kwa sasa anacheza soka katika club ya Shanghai SIPG ya China kuhusu nafasi yake ya kucheza timu yake ya taifa ya Brazil.

Oscer leo ameulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na maamuzi yake ya kwenda kucheza soka China haoni yamehatarisha nafasi yake ya kuitwa katika kikosi cha timu yake ya Brazil kitakachoshiriki Kombe la dunia 2018 nchini Urusi?

“Sijali kama nitaitwa kwenda kucheza Kombe la dunia au nisipoitwa maana sitaki kubaki masikini nitakapo zeeka halafu nibaki katika kumbukumbu kuwa niliwahi kucheza Kombe la dunia”>>> Oscer

Oscer aliamua kuondoka Chelsea mwaka 2016 na kwenda kujiunga na Shanghai SIPG ya China na kuingia katika list ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa duniani, hiyo ni baada ya kudumu Chelsea kwa miaka minne pekee, hivyo kwenda kwake kucheza China ni kwa sababu ya pesa.

UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu baada ya sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry

Soma na hizi

Tupia Comments