Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Haji Manara amemgeukia kipa wa Yanga

on

Afisa habari wa Simba Haji Manara ambaye amekuwa na utamaduni wa kupenda kuwatania watani wao wa jadi Yanga kupitia account zake za mitandao ya kijamii na imekuwa kama kitu cha kawaida.

Leo kupitia ukurasa wa instagram wa Haji Manara ameandika ujumbe wa kumkosoa golikipa wa Yanga raia wa Cameroon Youthe Rostand baada ya kutumia kauli mbiu ya Simba na kuandika “Yanga Nguvu Moja”

Baada ya kuona hivyo Haji Manara akaandika hivi “Nilisema wazi ipo siku kila mtanzania atashabikia Simba…imekuwa desturi kwa sasa kipa huyu wa Yanga kutumia kauli mbiu yetu..NGUVU MOJA…ile daima kuna mwiko nyuma kuna upawa haitaki kabisa!!”

Inawezekana Rostand kutokana na ugeni wake akawa hafahamu kuwa kauli ya “Nguvu Moja” ya Simba SC na ameichukulia kama ni usemi wa kawaida tu lakini kauli mbiu ya Yanga wao ni “Yanga daima mbele nyuma mwiko”

VIDEO:Magoli ya Simba walivyorudi kimataifa leo vs Gendermarie Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments