Michezo

VIDEO: Diego Maradona akimbizwa hospitali baada ya game Argentina vs Nigeria

on

Mkongwe wa soka wa Argentina Diego Maradona alikuwa sehemu ya zaidi ya mshabiki elfu 60 waliokuwa wamejitokeza katika uwanja wa Krestovski kufuatilia game ya mwisho ya Kundi D kati ya Argentina dhidi ya Nigeria mchezo ambao ulikuwa ni lazima Argentina apate matokeo.

Game hiyo ambayo Argentina alikuwa analazimika kushinda ili aingie hatua ya 16, walifanikiwa kushinda kwa kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Argentina yakifungwa na Lionel Messi dakika ya14, Marcos Rojo dakika ya 86 wakati goli la Nigeria lilifungwa na Victor Moses dakika ya 51 kwa mkwaju wa penati.

Presha ya mchezo inadaiwa kuleta presha kwa Maradona ambaye alikuwa akifuatilia mchezo ambapo dakika zikiwa zinaenda pasipo Argentina kupata goli hadi dakika ya 86 Marcos Rojo alipofunga, hivyo Maradona alinaswa katika video fupi akishindwa kutembea baada ya game na kupewa huduma ya kwanza na baadae kukimbizwa hospitali, bado haijawekwa wazi tatizo lake lakini linahisiwa na presha ilitokana na mchezo huo.

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments