AyoTV

“Hii sio timu ya kuibeza wala masihara” – MKWASA

on

Jumanne ya March 6 2018 Mabingwa wa Tanzania club ya Yanga watacheza mchezo wao wa kwanza wa club Bingwa Afrika round ya pili dhidi ya Township Rollers ya Botswana uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga anafuzu kucheza na Township Rollers baada ya kuitoa St Louis ya Shelisheli.

Kwa upande wa Township Rollers kesho watacheza na Yanga uwanja wa Taifa baada ya kuwatoa El Merreikh ya Sudan katika round ya awali, hivyo kuelekea mchezo huo, hivyo kuelekea mchezo huo Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa ameongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa Township Rollers sio timu ya kubeza.

“Kikubwa hasa ni kuwajulisha watanzania kuhusiana na mchezo wetu wa CAF Champions League, sisi tuna mechi kesho na tumuombe Mungu atusaidie ili tuweke mazingira ya kuingia katika makundi, hii sio timu ya kuibeza ipo vizuri kiuchumi na imeitoa El Merreikh ambao huwa wanafanya vizuri Champions League”>>>Mkwasa

VIDEO: Naibu waziri alivyoeleza sababu za kumfungia Roma na kumpa onyo Nay wa Mitego

Soma na hizi

Tupia Comments