Michezo

Kevin De Bruyne ametaja kwa nini hawezi kushindana na MO Salah tuzo ya PFA

on

Pamoja na kuwa watu na wadau mbalimbali wa soka England wamekuwa wakiwashindanisha kwa karibu kiungo wa Man City Kevin De Bruyne na winga wa Liverpool Mohamed Salah katika mbio za kuwania tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka, Kevin De Bruyne yeye amekuwa na mawazo tofauti.

Kevin De Bruyne

Kevin De Bruyne ambaye ameonekana kuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Man City kilichochini ya Pep Guardiola na kufanikiwa kutangazwa mabingwa wa EPL jana April 15, amekiri kuwa hawezi kushinda mbele ya Mohamed Salah katika kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kutokana na Mohamed Salah ana magoli mengi zaidi yake.

Mohamed Salah

Kwa upande wa Mohamed Salah ambaye tayari ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza EPL kuwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa EPL mara nne kwa msimu mmoja, amekuwa na msimu mzuri katika EPL kwani amefunga magoli 30 katika game 32 za EPL alizoichezea Liverpool ila De Bruyne amefunga magoli 7 na kutoa assist 15 msimu huu.

“Ndio nafikiri kama unachagua mshindi wa tuzo hiyo nje ya kikosi chetu basi Salah anastahili kiukweli kushinda tuzo hiyo kwa namna yoyote ile, ajabu kushindana na mtu ambaye amefunga magoli mengi zaidi yako ni wazi huwezi kushinda lakini binafsi nimeridhishwa na kiwango changu nilichokionesha msimu huu”>>> Kevin De Bruyne

ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1

Soma na hizi

Tupia Comments