Michezo

Gattuso kuhusu Buffon kuzozana na refa “Nimefanya matukio ya ajabu zaidi ya Buffon”

on

Moja kati ya stori ziliyochukua headlines wiki iliyomalizika ni game ya marudiano ya robo fainali ya michuano ya UEFA Champions League kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Game hiyo ilimalizika kwa Juventus kupata ushindi wa magoli 3-1. Goli la Real Madrid lilipatikana kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Cristiano Ronaldo dakika za nyongeza lakini golikipa wa Juventus Gigi Buffon hakukubaliana na maamuzi ya refa kiasi cha kufikia kuoneshwa kadi nyekundu.

Juventus licha ya ushindi wa magoli 3-1 wameondolewa katika michuano hiyo kwa aggregate ya jumla ya magoli 4-3 huku goli la penati la Real Madrid likachukua headlines juu ya upatikanaji wake wa penati, staa wa zamani wa AC Milan ambaye ni kocha wa timu hiyo kwa sasa Gennaro Gattuso ambaye alikuwa mtata enzi zake alipoulizwa mtazamo wake kuhusu kitendo Buffon kuzozana na refa Oliver alijibu

“Nimeshafanya matukio ya ajabu zaidi ya hilo la Buffon lakini Buffon atabakia kuwa Buffon kwa upande wangu nikiwa uwanjani niko tayari kupambana na mtu yoyote hata baba yangu mzazi kama inamaanisha ni kuitafutia ushindi timu yangu”>>> Gattuso

ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1

Soma na hizi

Tupia Comments