Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA: Baada ya kuipa kipigo Yanga, Simba sasa inahitaji point 5 tu!!!

on

Jumapili ya April 29 2018 mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga SC ulichezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huo ukiwa ni mchezo ambao ulikuwa unatazamiwa kutoa taswira ya Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018.

Simba leo wamefanikiwa kuondoka na point zote tatu baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0, goli la Simba limepatikana dakika ya 37 kupitia kwa Erasto Nyoni aliyetumia vyema pasi ya Shiza Kichuya.

Ushindi huo sasa unaifanya Simba ambayo imecheza michezo 26 ya Ligi na kusaliwa na michezo minne, ili iwe Bingwa bila ya kujali matokeo ya timu nyingine inahitaji point tano yaani ishinde mchezo mmoja na itoke sare mchezo mmoja, wakati Yanga wao kutetea Ubingwa wao kunategemeana na Simba apoteze mechi tatu huku yeye akipata matokeo chanya.

VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao

Soma na hizi

Tupia Comments