MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Okwi amefikia rekodi ya Bocco na Tambwe leo

on

Club ya wekundu wa Msimbazi Simba leo April 16 2018 ilikuwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mchezo wake wa 24 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya.

Simba wakiwa katika uwanja wa Taifa ambao ndio wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli ya Simba yakifungwa na nahodha wao John Bocco dakika ya 35 na Emmanuel Okwi dakika ya 80 kwa mkwaju wa penati baada ya Bocco kuchezewa faulo.

Ushindi huo unaendelea kuiweka Simba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Yanga kwa tofauti ya point 11 dhidi ya Yanga wanaowafuatia kwa kuwa na jumla ya point 47 ila Simba imeizidi Yanga michezo miwili.

Takwimu za game ya Simba vs Prisons baada ya dakika 90 kumalizika.

Hata hivyo kufunga kwa Emmanuel Okwi goli la pili dakika ya 80 kunamfanya Okwi kufikisha jumla ya magoli 19 ya VPL msimu huu lakini amefikia rekodi ya John Bocco aliyoiweka akiwa Azam FC na Amissi Tambwe ya kufunga magoli 19 kwa msimu lakini Okiwi ana nafasi ya kuvunja rekodi hiyo kwani zimebakia game sita VPL kumalizika.

Matokeo ya game za leo za VPL.

Msimamo wa VPL ulivyo kwa sasa baada ya game za leo kuchezwa.

ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1

Soma na hizi

Tupia Comments