Biko


Tangaza Hapa Ad

Top Stories

KALI YA MTWARA: Bi Harusi kaolewa Ijumaa, kaachika Jumamosi kwa sms

on

Hekaheka ya Leo Tena ya Clouds FM leo August 22, 2017 imetokea katika Mji wa Mikindani, Mtwara ambako mwanamke mmoja kaolewa Ijumaa kisha Jumapili akapewa talaka kwa njia ya massage.

Inadaiwa kuwa baada ya kufunga ndoa Ijumaa, siku iliyofuata yaani Jumamosi waliamka pamoja na mume wake na kuandaa chai wakanywa pamoja na chakula cha mchana pia wakala pamoja lakini ilipofika jioni akatumiwa talaka kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi.

Bibi harusi huyo anadai kuwa sababu alizopewa na mume wake ni kuwa mume wake huyo alikuwa na mwanamke mwingine hivyo angejiua kama angeoa mwanamke mwingine.

Aidha, kabla ya hapo familia zote zilikubaliana mwanaume aoe mke wa pili licha ya upande wa mke mkubwa wakipinga kwa madai walitaka mtoto wao ajifungue.

Bibi Harusi huyo alisema alikuwa anajua kuwa mume wake ana mke mwingine lakini matokeo yake amelala na mumewe usiku mmoja tu na siku iliyofuata alipewa talaka.

Mama mtu mzima aliyepigwa Kariakoo akidaiwa kuiba dera asimulia 

Bonyeza PLAY hapa chini kumsikiliza Bibi Harusi aliyeachika..

HEKAHEKA: Mwanamke adaiwa kumkata sehemu za siri mtoto wa jirani yake…kisa?

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement