Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Niyonzima baada ya Bocco kuipatia ushindi Simba leo

on

Wekundu wa Msimbazi Simba Jumamosi ya December 30 walikuwa Nangwanda Mtwara kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji wao Ndanda FC wanakuchele, Simba wakiwa Mtwara walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0.

Niyonzima

Magoli ya Simba yote mawili yalifungwa na John Bocco dakika ya 52 na dakika ya 56, baada ya ushindi huo, kiungo wa Simba raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa majeruhi alitumia ukurasa wake wa instagram kueleza furaha yake hasa uwezo wa Bocco aliouonesha.

“Alhamudulilah kwa ushindi wa leo na pia ongera sanaa wachezaji wote,kiukweli siku ya leo imekuwa siku nzuri yenye furaha na amani,big up my brother Bocco Mungu azidi kukusimamiya mwanangu.Simba nguvu moja ?? najua wataelewa one day”>>>Niyonzima

“Nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba”-Haji Manara

Soma na hizi

Tupia Comments