Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

U HEARD: Ommy Dimpoz na Alikiba wadaiwa kuiga Video ya Harmonize

on

Kwenye U Heard ya Clouds FM leo mtangazaji wa XXL Soudy Brown ameileta hii stori kuhusu mazingira iliporekodiwa Video mpya ya Ommy Dimpoz na Alikiba, Kajiandae kufanana na mazingira ya Video ya Bado ya Harmonize zote zikiwa zimefanywa South Africa.
whatsapp-image-2016-11-17-at-4-59-04-pm

Soudy Brown amezungumza na Ommy Dimpoz ili kujua nini kilifanyika mpaka wakaamua kwenda kushoot eneo lilelile ilipofanyika Video ya Harmonize – Bado na kuna taarifa Ommy na Alikiba waligoma kuendelea kushoot. Kajiandae ni Video mpya ya wimbo wa ushirikiano kati ya Ommy Dimpoz na Alikiba.

Kwa mujibu wa Ommy Dimpoz amesema kuwa mwanzo hawakujua kama mazingira yale ndiyo yaliyofanyika video ya Harmonize mpaka walipofika eneo la kufanyia kazi na wakaamua kumuuliza muongozaji kwanini amechagua eneo ambalo tayari kuna video imeshafanyika.

“Nani alisusa? hamna kitu kama hicho unajua waongozaji wa hizi Video mbili ni tofauti sisi tulivyoenda kwanza ilikua kuna sehemu tushoot mchana kwahiyo mimi nilikuwa sijakagua location tulikua tumetumiwa tu kwenye picha. Nilivyofika kuona location nikamwambia Director mbona hapa pameshatumika kutakuwa hakuna tofauti, Campos akaamua kushoot usiku ili kutofautisha. – Ommy Dimpoz

Kuipata full stori bonyeza play hapa chini kusikiliza.

 

VIDEO: Babu Tale alivyozungumzia ukaribu wa Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz, Tazama hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement