PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

AyoTV

EXCLUSIVE: Kwa nini Msuva hajafika Taifa Stars hadi leo? sababu kataja hapa

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku wa Jumanne ya October 9 2018 ndio itaondoka Tanzania kuelekea Cape Verde kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya fainali za michuano ya Africa AFCON 2019 nchini Cameroon.

Taifa Stars ambayo itacheza mchezo huo dhidi ya Cape Verde October 12 hadi sasa winga mshambuliaji wake Simon Msuva anayecheza Difaa El Jadid ya Morocco hajawasili Dar es Salaam kwa ajili ya kuungana na wachezaji wenzake.
Msuva ni miongoni mwa wachezaji wa nje ambao hawajawasili bado akiwemo Mbwana Samatta ambaye usiku wa jana alikuwa na kazi ya kuitumikia Genk katika mchezo dhidi ya KAA Gent uliyomalizika kwa Genk kushinda magoli 5-1, Msuva amesema ataungana na timu Cape Verde kwa sababu kutoka Casablanca Morocco alipo yeye ni mwendo wa saa nne hadi Cape Verde.

“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments