DSTV


Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Kitu Samatta kaongea kabla ya kucheza na Malawi kesho

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo Ijumaa ya October 6 2017 imefanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Uhuru kabla ya kucheza mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki uliyopo katika kalenda ya FIFA dhidi ya timu ya taifa ya Malawi.

Taifa Stars inacheza na Malawi kwa mara nyingine baada ya kucheza nao katika mchezo wa COSAFA, katika viwango vya FIFA Taifa Stars ipo nafasi ya 125 wakati na Malawi wao wapo nafasi ya 116, kuelekea game hiyo nahodha mkuu wa Taifa Stars Mbwana Samatta amefunguka.

“Mimi nafikiri Malawi tunawafahamu na ndio kitu ambacho kitaleta ugumu kwa sababu tumecheza nao mara nyingi sana, lengo ni kushinda katika mchezo wa kesho ili kupanda katika viwango vya FIFA, huwezi kucheza nyumbani halafu uwaambie watanzania wasiwe na matarajio makubwa” >>> Samatta

Cristiano Ronaldo ameuza tuzo yake ya Ballon d’Or 2013

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement