Habari za Mastaa

Alicios Theluji avutiwa na mchekeshaji Idris Sultan (+video)

on

Msanii wa muziki kutoka DRC Congo ambaye anafanya shughuli zake za muziki nchini Kenya Alicios Theluji amemuongelea mchekeshaji Idris Sultan na kusema kuwa anavutiwa naye na ni mchekeshaji mzuri hata katika maisha ya uhalisia.

Alicios Theluji ameyaongea hayo kupitia mahojiano aliyoyafanya katika kituo cha radio cha Citizen kupitia kipindi cha Mseto East Africa na mtangazaji Willy Mtuva hata hivyo msanii huyo ametaja vigezo vya mwanaume anayemtaka ili aweze kuendana nae katika mahusiano ya kimapenzi.

“Mimi crush wangu huwa wanabadilika kila mara lakini ninaye crush kutokea hapahapa Nairobi lakini nitamtaja mmoja kutokea Tanzania ambaye ni Idris Sultan anachekesha hata katika maisha ya kihalisia” >>>Alicios 

VIDEO:Account ya Marehemu Godzilla instagram yageuzwa page ya umbea

Soma na hizi

Tupia Comments