Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kichuya ameipatia point tatu Simba dhidi ya Azam FC

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena Jumamosi ya Septemba 17 2016 kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja sita tofauti, moja kati ya mchezo uliochezwa ni Azam FC waliwakaribisha Simba katika dimba Uhuru Dar es Salaam, katika mchezo ambao kila mmoja alikuwa anawania kupata ushindi ili apate nafasi ya kuongoza.

img_0067

Huu ulikuwa ni mchezo unazikutanisha timu ambazo zote zilikuwa na point 10 na wastani wa magoli ya kufunga na kushinda walikuwa wapo sawa, haukuwa mchezo rahisi kuona timu ikiruhusu kufungwa kwani hadi dakika ya 45 za kwanza zinamalizika walikuwa 0-0.

img_0044

Kipindi cha pili dakika ya 67 Simba wakabadili ubao wa matokeo na kuufanya usomeke 1-0 baada ya Shiza Kichuya kufunga goli la ushindi kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Azam FC Aishi Manula, Simba sasa atashuka dimbani Septemba 24 kucheza dhidi ya Majimaji katika uwanja wa Uhuru, wakati Azam FC watakuwa Mtwara kucheza na Ndanda FC.

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement