Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Rapper Chemical aeleza kilichokwamisha movie yake na Wema Sepetu

on

Rapper wa kike na mwanafunzi wa UDSM, Chemical leo Dec 22, 2016 ameeleza sababu zilizokwamisha album yake pamoja na movie mpya aliyomshirikisha mwigizaji Wema Sepetu.

Rapper huyo akizungumza na millardayo.com & Ayo TV aliyaongea haya>>>‘Labda naweza kusema nilikuwa nimepanga kuachia album mimi na mwenzangu ila kutoka na mimi kubanwa na masomo chuoni sikuweza kukamilisha album hiyo ambayo sasa hivi ingekuwa madukani’

‘Kitu kingine ambacho nilikuwa nimepanga ni kuachia movie mpya ya Wema ambayo tulikuwa tumepanga kuitoa mwaka 2016 tumeshoot tangu mwezi wa 11 lakini ndio hivyo mambo hayajakamilika kwasababu shule inabana’

‘Kama utakuwa umesikiliza wimbo wangu wa Mary Mary ni wimbo ambao unahusiana na watoto wa mtaani kwahiyo tukaona tuilete kwenye movie ili stori iwe nzuri mtu anapoona kile nilichokiimba kwenye hiyo movie’

Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Chemical akieleza kilichokwamisha movie yake na Wema Sepetu

ULIIKOSA HII YA SHILOLE NA MPENZI WAKE WALIVYOJIACHIA KWENYE BIRTHDAY PARTY BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement