PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Kweli Baba Isaya kadhamiria kurudi Ligi Kuu

on

Ligi daraja la kwanza imeanza leo kwa michezo kumi kuchezwa lakini moja kati ya michezo iliyochezwa leo ni mchezo kati ya Arusha United dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora, game imechezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Club ya Arusha United inayofundishwa na kocha mahiri wa kupandisha timu Ligi Kuu Fred Felix Minziro AKA Baba Isaya, ikiwa nyumbani Arusha imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza kwa kuifunga Rhino Rangers ya Tabora kwa magoli 2-1.

Fred Felix Minziro

Ushindi huo umedhihirisha utabiri wa wengi kuwa Fred Feliz Minziro amedhamiria kuileta timu ya Arusha United katika Ligi Kuu 2019/20, hiyo ni kutokana na kuanza vye michuano hiyo leo, baada ya kuweka kambi Karatu.

Kama ufahamu ikifanikiwa kocha Minziro akaipandisha timu ya Arusha United kucheza Ligi Kuu msimu wa 2019/20 atakuwa anaweka rekodi ya kupandisha timu tatu mfululizo Ligi Kuu, baada ya msimu mwaka juzi kuipandisha Singida United, msimu wa mwaka jana kuipandisha KMC  ya Kinondoni na sasa anaipambania Arusha United.

JB na Ray “Hata Yanga wao wanajua Simba ana timu bora”

Soma na hizi

Tupia Comments