AyoTV

Canavaro baada ya Yanga kutolewa Mapinduzi “timu yenyewe imebakia Dar”

on

Club ya Yanga SC usiku wa January 7 2019 imeyaaga rasmi mashindano ya Mapinduzi Cup 2019 baada ya kupokea kipigo cha pili katika michuano hiyo, Yanga ilikuwa inacheza dhidi ya Malindi SC katika uwanja wa Amaan Zanzibar, hiyo ikiwa ni game yake ya tatu Kundi B.

Yanga ambao kikosi chao cha kwanza wamekiacha Dar es Salaam kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu na kuleta Zanzibar kikosi cha team B na wachezaji baadhi wakikosi cha kwanza, wamejikuta wakipokea kipigo cha magoli 2-1 na kuyaaga mashindano hayo, meneja wa Yanga Nadir Haroub Canavaro aliongea na waandishi wa habari.

“Tunamshukuru Mungu tumemaliza vizuri na baadhi ya vijana wamepata uzoefu nawapongeza Malindi kwa kuweza kushinda makosa tulioyafanya ndio waliyoyatumia kama tulivyofanya makosa kwenye mechi na Azam bado tuna mchezo wetu wa mwisho tunamalizia ili kurudi Dar kujiandaaa na Ligi sababu timu yenyewe imebaki Dar”>>>Nadir Haroub

Mbona Jonas Mkude hatumuoni Zenji? Meneja wa Simba kajibu

Soma na hizi

Tupia Comments