Michezo

Jose Mourinho alivyopaniki baada ya Chelsea kushangilia mbele yake

on

Jumamosi ya October 20 Man United ilikuwa mgeni wa Chelsea katika Ligi Kuu England, game ambayo ilichezwa katika uwanja wa Stamford Bridge, Man United haikuwa ikitarajiwa kufanya vizuri sana katika mchezo huo.

Man United wakiwa ugenini walianza kuruhusu goli dakika ya 21 baada ya Rudiger kufunga goli la uongozi lakini dakika ya 55 na 73 Anthony Martial akaifungia Man United goli la kusawazisha na baadae goli la uongozi.

Chelsea walilazimika kusubiri hadi dakika za nyongeza ambapo Barkley akafanikiwa kuisawazishia Chelsea goli na kufanya mchezo kumalizika kwa kufungana magoli 2-2, baada ya Chelsea kusawazisha Mourinho alikasirishwa na kitendo cha kocha msaidizi wa Chelsea Marco Ianni  kushangilia goli mbele yake.

Hata hivyo kocha wa Chelsea Maurizio Sarri aliomba radhi kwa kitendo hicho na kusema kuwa staff wake hakufanya kitu sahihi kushangilia mbele ya Mourinho “Halikuwa kosa langu ni msaidizi wa Sarri usifanye kitu ambacho kila mmoja anafanya na kusema lakini wameniomba msamaha kila kitu kipo sawa”>>>Mourinho

Samatta alivyofutwa miguu baada ya game

Soma na hizi

Tupia Comments