Michezo

Chirwa alivyopokewa na kutambulishwa Azam FC leo

on

Club ya Azam FC leo ilitangaza rasmi kuingia mkataba na mshambauliaji wa zamani wa Yanga rai wa Zambia Obrey Chora Chirwa, hivyo tutarajia kumuona staa huyo kuanza kuitumikia club hiyo hivi karibuni baada ya kushindwa kukamilisha dili lake na Yanga SC.

Chirwa sasa baada ya kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC baada ya kocha Hans van Pluijm kupendekezwa aongezwe kikosini, staa huyo atakuwa anakamilisha idadi ya wachezaji 27 wa Azam FC watakaopambania taji la Ligi Kuu msimu wa 2018/2019.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Obrey Chirwa kabla ya kutangazwa kujiunga na Azam FC aliwahi kuichezea Yanga SC na baadae akaenda Misri kucheza soka kabla ya kuvunja mkataba na club hiyo na kurejea Tanzania na kujiunga na Azam FC.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments