Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA 7: Simba imepata ushindi vs Toto kwa mara ya kwanza baada ya mechi 6

on

Baada ya Jumamosi ya October 22 2016 kuchezwa michezo baadhi ya Ligi Kuu soka Tanzania bara, Jumapili ya October 23 2016 ilichezwa michezo ya miwili ya Ligi Kuu, wekundu wa Msimbazi Simba wao walikuwa wenyeji wa Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wao wa 11 wa VPL msimu wa 2016/2017.

dsc_0036

Kabla ya mchezo wa leo kuchezwa Simba alikuwa kacheza na Toto Africans katika mechi sita zilizopita bila kupata ushindi zaidi ya kupoteza mara mbili na kupata sare nne, mchezo wao wa mwisho Simba kucheza na Toto Africans ilikuwa 17/4/2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam na walikubali kipigo cha goli 1-0.

dsc_0027

Leo October 23 2016 Simba imefanikiwa kuvunja rekodi yao mbaya dhidi ya Toto Africans kwa ushindi wa goli 3-0, magoli ya Simba yalianza kufungwa na Mzamiru Yasini dakika ya 43 baada ya kupokea assist ya Fredrick Blagnon na akafunga goli la tatu dakika ya 74, hiyo ni baada ya Laudit Mavugo kufunga goli la pili dakika ya 52 kwa kutumia vyema pasi ya Ibrahim Mohamed.

dsc_0021

dsc_0040

dsc_0012

dsc_0068

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement