AyoTV

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

on

Mfanyabiashara na muwekezaji wa club ya Simba SC Bilionea Mohammed Dewji alikuwa sehemu ya mashabiki waliojitokeza uwanja wa Taifa Dar es Salaam kushuhudia mchezo wa Simba SC dhidi ya Mbabane mchezo wa CAF Champions League round ya kwanza.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mohammed Dewji kuonekana uwanja wa Taifa Dar es Salaam, toka atekwe October 11 2018 akiwa maeneo ya Gym nje ya Hotel ya Colleseum, Dewji leo ndio ameonekana ikiwa ni siku 49 toka atekwe na amepokewa na shangwe na mashabiki wa Simba SC.

EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?

Soma na hizi

Tupia Comments