PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Style ya kushangilia ya Paul Pogba inamkwaza Claude Makele

on

Mkongwe wa Ufaransa Claude Makelele ameamua kutia neno kuhusu mchezaji Paul Pogba anayeichezea Man United, Makelele ameamua kutia neno kuhusiana na style ya ushangiliaji ya mchezaji huyo ambayo amekuwa akiitumia kwa sasa anapoifungia Man United.

Paul Pogba kwa sasa amekuwa akifunga magoli na hivi karibuni alifunga magoli mawili ya Man United katika ushindi wa 4-1 dhidi ya AFC Bournemouth, hivyo Makelele ameeleza kuwa kama angekuwa bado anacheza basi angeongea na Paul Pogba katika vyumba vya kubadilishia nguo kuwa style yake ya kushangilia inamvunjia heshima mpinzani wake.

Hivyo anahisi anapaswa kushangilia vile akiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo lakini uwanjani ashangilie kwa kawaida tu ili kuonesha heshima kwa wapinzani wao, Makele alifika mbali zaidi kuwa wakati anacheza soka hata Thierry Henry aliwahi kuwa anashangalia kwa namna ambayo haimuheshimu mpinzani lakini alimkataza.

“Moja kati ya mfano huo alikuwa ni Thierry Henry alipokuwa akifunga goli kila mmoja alikuwa anamshangaa, siku nikamuuliza Henry kwa nini unafanya vile akanijibu ndio namna ninavyoshangilia goli langu najua watu hawapendi lakini mimi napenda ndivyo ninavyoshangilia goli langu siwezi kubadilisha, kwangu mimi ilikuwa ni kama umuheshimu mpinzania”>>>Makelele

Kocha wa Simba baada ya kuwasili Zanzibar”Sio njia bora ya kuandaa timu”

Soma na hizi

Tupia Comments