Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Galatasaray imekubali kumuokoa Eboue katika wazo la kujiua

on

Siku moja imepita toka staa wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast aliyekuwa anavichezea vilabu vya Arsenal na Galatasaray Emmanuel Eboue atangaze kuwa amefilisika kutokana na mkewe kuchukua mali zote na kukiri kuwa limewahi kumjia wazo la kujiua.

Eboue ameripotiwa kuwa baada ya kutalakiana na mkewe aliyekuwa amezaa nae watoto watatu, amepoteza utajiri wake wote kutokana wakati alipokuwa anacheza soka kila utajiri wake wote alikuwa kamuandikisha mkewe kitu ambacho kinamgharimu kwa sasa.

Staa huyo amekiri kufilisika na kukosa pesa za kulipa wanasheria ili kumtetea lakini amefikia kukosa hata pakulala na pesa ya kupeleka nguo dry cleaner hivyo alilazimika kuwa anafua kwa mkono, siku moja baada ya taarifa hizo kutoka huku Eboue akitangaza kuomba msaada.

Club ya Galatasaray ya Uturuki ambayo amewahi kuichezea kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kuondoka Arsenal mwaka 2011, imetangaza kumpa kadhi ya ukocha msaidizi wa timu ya U-14 ya Galatasaray, kumpa makazi na kumlipa mshahara utakaomuwezesha kujikimu na kuishi vizuri.

“Nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba”-Haji Manara

Soma na hizi

Tupia Comments