PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

UEFA imemuadhibu rasmi Ronaldo kwa style yake ya ushangiliaji

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika club ya Juventus ya Ureno Cristiano Ronaldo kutokana na awali kudaiwa kuwa atakutana na wakati mgumu kutoka UEFA ambao walikuwa wamemfungilia shitaka katika kamati ya maadali kutokana na style yake ya ushangiliaji dhidi ya Atletico Madrid, leo kaadhibiwa kweli

Ronaldo ambaye aliifungia Juventus magoli matatu (hat-trick) 3-0 dhidi ya Atletico Madrid katika come back 2-0 waliyofungwa katika mchezo wao wa kwanza wa 16 bora ya UEFA Champions League, amefunguliwa mashitaka na kuanza kuchunguzwa na UEFA kutokana na style yake hiyo.

UEFA leo baada ya kukaa na kujadili kupitia kamati zao zimeamua kumpiga faini Cristiano Ronaldo ya euro 20000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 53, kwa kukutwa na hatia ya ushangiliaji wake ambao baadhi ya watu unawakosea heshima, Ronaldo inadaiwa alifanya hivyo kama kumjibu kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ambaye alishangilia kwa style hiyo pia.

Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!

Soma na hizi

Tupia Comments