Biko


Tangaza Hapa Ad

Burudani

Diamond na Producer Tudd Thomas washinda tuzo za AELA Nigeria

on

Muimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz pamoja na producer Tudd Thomas wamefanikiwa kushinda tuzo za African Entertainment Legends Awards (AELA) zilizofanyika  usiku wa Desemba 3, 2017 Lagos nchini Nigeria.

Diamond Platnumz ameshinda tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana Afrika kupitia wimbo wake wa Fire aliyomshirikisha Tiwa Savage kutokea nchini Nigeria,  wakati producer Tudd Thomas kutokea Tanzania akishinda tuzo ya producer bora wa Afrika kwa mwaka 2017.

Tuzo hizo zinazofanyika kila mwaka nchini Nigeria Diamond alikuwa akishindanishwa na Fally Ipupa x Booba – Kinane [Congo], Davido x Nasty C – Coolest kid in Africa (Nig/SA) Runtown x Sarkodie –Painkiller (Nig/Ghana) C4 Pedro x Sautisol – Love again (Angola/Kenya) Illbliss x Runtown – I can’t hear you (Nig) Wizkid x Drake – Come Closer (Nig/ USA) Phyno x Wande – Zamo Zamo (Nig) Babe Wodumo x Mampinsta –Wololo (SA).

VIDEO:”Wema Tuko Vizuri kama ulivyotuacha, CCM sio kama Basi” Richie Richie

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement