AyoTV

Simba SC imepindua matokeo vs Al Ahly, point tatu muhimu Taifa

on

Baada ya club ya Simba SC kupokea vipigo viwili mfululizo vya magoli 5-0 jijini Kinshasa dhidi ya AS Vita na Alexandria nchini Misri dhidi ya Al Ahly leo ilikuwa inacheza game ya marudiano dhidi ya Al Ahly uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ikiwa kama mashabiki wa Simba wamekata tamaa kwa vipigo vya kutisha.

Simba SC leo wakiwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam dhidi ya Al Ahly wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere dakika ya 65 na kujikusanyia point tatu zilizowafanya wafikishe jumla ya point 6, huku Al Ahly wakiwa wanaendelea kuongoza Kundi lao D wakiwa wamesalia na point zao 7.

Hadi sasa tukiwa tunasubiri mchezo wa JS Saoura dhidi ya AS Vita utakaochezwa saa 22:00 usiku leo nchini Algeria, msimamo wa Kundi D Al Ahly ndio anaongoza kwa point 7, akifuatiwa na Simba SC kwa point 6, AS Vita kwa point 4 wakiwa nafasi ya tatu na JS Saoura wakushika mkia kwa kuwa na point 2.

“Sijui walitudharau, Tumewaonesha sisi sio timu kutoka vijijini”-Kocha Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments