Michezo

CAF imemteua Mtanzania kuwa kamishna wa mchezo wa fainali

on

Mtanzania Lina Kessy ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kusimamia mchezo wa Fainali ya Afrika kwa Wanawake, Lina atakuwa Kamishna wa mchezo huo wa Fainali utakaochezwa Kesho Jumamosi Disemba 1,2018 utakaowakutanisha Nigeria dhidi ya Afrika Kusini.
Mchezo huo namba 16 utachezwa Accra Sports Stadium saa 10 jioni, fainali hiyo itachezeshwa na mwamuzi kutoka Zambia Glady Lengwe atakayesaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 kutoka Madagascar Lidwine Rakotozafinoro, Mwamuzi msaidizi namba 2 Bernadettar Kwimbira kutoka Malawi na Mwamuzi wa akiba Fatou Thioune.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
tunamtakia kila la heri Lina Kessy tunaamini uwezo wake wa kusimamia michezo mikubwa kama huo wa Fainali ya Afrika kwa Wanawake.
IMETOLEWA NA TFF
EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?
https://youtu.be/RSeYrwNEO9M

Soma na hizi

Tupia Comments