PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Habari za Mastaa

Anko Zumo- ‘’Tulikuwa hatufikirii kama Mai Zumo atakuwa mwigizaji siku moja”

on

Mchekeshaji Anko Zumo amefanya mahojiano na kipindi cha radio cha Leo Tena cha Clouds FM amezungumza vitu vingi ikiwemo mwanae Mai kuwa miongoni mwa waigizaji anaofanya nao kazi na kusema kuwa ni kitu ambacho hakutegemea kuwa mwanae atakuwa muigizaji.

>>>‘’Tulikuwa hatufikirii kama Mai Zumo atakuwa mwigizaji siku moja naye alitaka kuonekana kwenye video tukamwambia atoke asilete fujo hadi tukashindwa kufanya shughuli yetu alikuwa analia tukamwabia afanye tulilomwambia akaweza vizuri tangu siku hiyo tukaanza kumtumia’’

>>>Kwenye familia yetu huwa tunachekeshana sana wenyewe kwa wenyewe, hasa tunapokutana kwenye shehere huko nyumbani kwetu, kuna siku nilipost kichekesho nilikuwa naogeshwa kwenye beseni kuna rafiki yangu alikiona alijua kuwa labda nimefumaniwa nikamwambia kilikuwa ni kichekesho akaniambia ninajua sana kuchekesha nivipost vichekesho kwenye instagram’’

>>>“Nilifunga ndoa na mke wangu Mama Mai @habibazumo kabla sijakuwa mwigizaji wa Vichekesho kipindi hicho nilikuwa fundi gereji.”

ROSA REE AMBWATUKIA SHABIKI YAKE “HAKIKISHA UNA TIKETI YA MBINGUNI”

Soma na hizi

Tupia Comments