PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Maamuzi waliyofikia familia ya rubani aliyepata ajali na Emiliano Sala

on

Ni siku mbili zimepita tokeo jopo la uokoaji na utafutaji wa ndege iliyokuwa imepotea ikiwa imewabeba mshambuliaji mpya wa Cardiff City Emiliano Sana na rubani David Ibbotson, kupatika ikiwa imeanguka chini ya maji na mwili mmoja kupatikana.

David Ibbotson

Mwili huo ulifanyiwa uchunguzi na kubaini kuwa ni mwili wa Emiliano Sala ila mwili wa rubani wake Mr David bado haujapatikana, ndege iliyokuwa imewabeba wawili hao kutoka Nantes Ufaransa kuelekea Cardiff ilipatikana na kuibuliwa ilipokuwa imezama chini ya maji ila rubani David Ibbotson hajaonekana.

Marehemu Emiliano Sala katika picha

Baada ya taarifa hizo kutoka na familia ya David Ibbotson kutojua ndugu yao yuko wapi licha ya kuhisiwa amepoteza maisha, imeamua kuchangisha pesa pound 63000 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 180 kwa ajili ya kuendesha zoezi la kumtafuta ndugu yao, hata hivyo familia hiyo imefikiria kuchangisha hadi wafikie pound 300000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 890 ndio zitasaidia kuendesha zoezi hilo.

David Ibbotson upande wa kushoto.

“Tunashindana na timu zenye nguvu, aliyetoa assist Alexandria kanunuliwa Bilioni 10”-MO Dewji

Soma na hizi

Tupia Comments